Na Bongo leaks
HALMASHAURI ya wilaya ya Iringa
imewafukuza kazi watumishi wake sita,
kutokana na makosa mbali mbali ikiwemo utovu wa nidhamu na utoro kazini.
Maamuzi hayo yamefikiwa katika
kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo, baada ya watumishi hao kwa
nyakati tofauti kupewa onyo na kalipio kali.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,
Steven Mhapa alisema katika kipindi chote cha utovu wa nidhamu watumishi hao
waliendelea kupokea mishahara yao kama kawaida.
“Ofisi ya Mkurugenzi ilileta rasmi
ombi la kuwafukuza kazi watumishi hawa, hivyo baraza la madiwani limebariki
kwani, hata sisi hatupo tayari kuona kazi zinalala kwa sababu za uvivu,”
alisema
Aliwataja watumishi hao kuwa ni
Andrew Mtavangu na Uswege Mwakosya waliokuwa Maafisa Elimu Wasaidizi Daraja la
Tatu na Prosper Mzena aliyekuwa Mwalimu.
Wengine ni Sabath Masembo
aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la Pili, Abdukadh Mnyavanu aliyekuwa
Mtendaji wa Kijiji na Godfrey Msuya aliyekuwa Tabibu Msaidizi.