AUWAWA NA WANANCHI BAADA YA KUIBA MAHINDI MATATU SHAMBANI WILAYANI KAHAMA


Mtu mmoja Hamisi Mayala anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 58 hadi 60 amefariki dunia baada ya kuuawa na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira kali katika kijiji cha Kilago wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kutokana na kusadikika kuwa ameiba mahindi mabichi.

Akizungumza Diwani wa Kata ya Kilago Peter Emanuel amesema Tukio hilo limetokea juzi Majira ya saa 12 jioni baada ya baadhi ya wananchi kumkuta akivunja mahindi katika shamba ambalo halijafahamika kuwa ni la Nani.

Amesema wananchi hao wakipiga kelele ndipo umati wa watu ulijaa na kuanza kumshambulia kwa silaha za jadi hadi kuumuua na kwamba wananchi walisambaa baada ya kuona mtuhumiwa huyo amepoteza maisha.

Diwani Emmanuel amesema amepata taarifa kutoka kwa viongozi wake wa kijiji, na kuchukua jukumu la Kupiga simu Polisi ambao wamefika jana asubuhi na Kuuruhusu mwili wa marehemu uzikwe kwa kuwa ndugu zake wahakufahamika mara moja.

Amesema Marehemu Mayala ameingia kijijini hapo mwaka Juzi na alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga huku akijishughulisha na kufanya vibarua kwa wakulima wa kijiji hicho na inadaiwa alitokea katika Tarafa ya Msalala Wilayani Kahama.

Hata hivyo Diwani Emmanuel amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na dabala yake wawafikishe watuhumiwa sehemu inayohusika, huku akiahidi kulisaidia jeshi la polisi kutoa elimu kwa wananchi.

Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukia hilo na linaendelea na Uchunguzi wa kuwabaini waliohusika na mauaji hayo ya kujichukulia sheria mkononi na kuwafikisha katika mikono ya sheria.
 
na Redio Kahama


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo