AMUUA MWENZAKE KWA KIPIGO KWA KUMTUHUMU KUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA MAMA YAKE

Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobius Sedoyeka, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mauaji ya watu wawili wakazi wa wilaya ya Ikungi akiwemo mmoja kuuawa kwa kutuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mama mzazi wa muuaji. Salumu Juma mkazi wa kijiji cha Makotea, amemuawa Faraja Emmanuel, kwa madai kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mama yake.(Picha na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu, Singida
MKULIMA mmoja na mkazi wa kijiji cha Makotea wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Salumu Juma (37) amefariki dunia baada ya kushambuliwa vibaya na Faraja Emmanuel  kwa tuhuma ya kuwa na mahusiano ya mapenzi na mama yake.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida,ACP Thobius Sedoyeka amesema tukio hilo limetokea aprili 19 mwaka huu saa saba mchana huko katika hospitali ya misioni ya Makiungu wilaya ya Ikungi.

Amesema siku ya tukio,mtuhumiwa Salumu alimvizia njiani Faraja na baada ya kumvamia alimshambulia kwa kutumia rungu sehemu mbalimbali za mwili  na kisha kumvunja miguu yote miwili.

“Salumu baada ya kutimiza azma yake hiyo alimwacha Faraja akiwa amezirai na yeye kulimbilia kusikojulikana wasamaria wema waliweza kumwokota Salumu na kisha kumkimbiza katika hospitali ya Makiungu ambapo alifariki akiwa anaendelea kupatiwa matibabu”,alifafanua zaidi,Sedoyeka.
Amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Salumu ametenda kosa hilo baada ya kuchukizwa na tabia ya Faraja kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mama yake mzazi.

“Kwa sasa tumeanzisha msako mkali wa kumtafuta Salumu ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Katika tukio jingine,Sedoyeka amesema kuwa Joram Joseph (36) mkulima na mkazi wa kijiji cha Msimii kata ya Sepuka wilaya ya Ikungi,amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu shingoni na bega la kushoto na baba yake mzazi Joseph Benjamin (61).
Amesema tukio hilo limetokea Aprili 21 mwaka huu saa moja usiku huko katika kijiji cha Msimii Sepuka.

Kaimu kamanda huyo amesema chanzo cha mauaji hayo ni kutokana na Joram kumtukana matusi ya nguoni baba yake mzazi.Joramu inadaiwa kutoa matusi hayo kutokana na kulewa pombe ya kienyeji kupindukia.

“Baada ya mauaji hayo,mtuhumiwa mzee Joseph aliweza kujisalimisha mwenye katika kituo cha polisi cha Sepuka”,amesema Sedoyeka.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo