WATU wawili wanashikiliwa na
jeshi la polisi mkoani Iringa kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi, kifuani Afisa
masoko wa kampuni ya Vinywaji ya Coca-Cola Mkoani Iringa, Steven Mbwilo (40).
Kaim Kamanda wa Jeshi hilo, mkoani Iringa Wakyo Nyigesa aliwataja watuhumiwa hao
kuwa ni Pascal Benedict (44), mkazi wa Tunduma na Selemani Juma (42) mkazi wa Soweto mkoani Mbeya.
Alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi, saa
sita mchana katika kijiji cha Mtiri, kata ya Ifwagi, Wilayani Mufindi ambapo
watu hao walimvamia afisa huyo na kumpiga risasi iliyosababisha kifo chake papo
hapo.
Hata hivyo, walisema kuwa
marehemu huyo baada ya kupekuliwa alikutwa na fedha Shilingi Milioni 4.7
sambamba na simu yake ya mkononi.
Aliongeza kuwa sababu za mauaji hayo
hazijajulikana na kwamba, uchunguzi zaidi unaendelea ili watuhumiwa hao
wafikishwe mahakamani kujibu shtaka linalowakabili.
