WAZAZI NA WALEZI WASIOTAKA WATOTO WAO KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA KUKIONA CHA MOTO

Serikali mkoani Geita imeanzisha mkakati wa kuwachukulia hatua za kisheria wazazi na walezi wasiotaka watoto wao wa kike kujiunga kidato cha kwanza, hatua inayofanyika kutokana na kuongezeka kwa wimbi la wazazi wasiotaka kuwaendeleza watoto wa kike wanaofaulu kujiunga na elimu ya sekondari kwa lengo la kuwaozesha.

Hatua ya msimamo huo wa serikali imefuata baada ya kutibitika kuwa maeneo mbalimbali kanda ya Ziwa yameshamili kwa vitendo hivyo ambavyo kimsingi vinachangia kurudisha nyuma juhudi za kumkomboa mwanamke ili aweze kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika shule ya sekondari ya Waja Springs iliopo mkoani Geita Mkuu wa wilaya hiyo Manzie Mangochie amethibitisha kuwa mwenendo wa elimu mkoani hapo hauridhishi licha ya wazazi wengi kutambua umuhimu wa elimu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo