WATANZANIA WANNE WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA.

Watanzania wanne (mwanaume mmoja na wanawake watatu) wamekamatwa na kilo 2.2 za heroin kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Watanzania hao waliingia nchini Kenya kupitia Namanga na walikuwa njiani kuelekea Hong Kong.

"Tumewakamata Watanzania wanne leo (jana) JKIA. Tumewaweka chini ya uangalizi na tayari wameshatoa vidonge 186 ambavyo tumevifanyia uchunguzi na kudhibitisha kuwa ni heroin," Ngisa aliliambia Shirika la Habari la Uchina kwa simu. 
 
Ameongeza kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo