Wananchi wakiwa wamemzunguka mtuhumiwa huyo wa wizi huku akiendelea kupigwa.Picha/habari na Eddy Blog Team.
=====
Wananchi
wenye hasira katika kata ya Tandala wilayani Makete mkoa wa Njombe
wameamua kujichukulia sheria mkononi, kwa kumpiga hadi kumuua kinyama
mtuhumiwa wa wizi ambaye walimkamata kwa madai kuwa ni mwizi wa mifugo
Tukio
hilo limetokea jana majira ya saa 11 jioni ambapo kwa mujibu wa
mashuhuda wa tukio hilo ambao walikataa kutaja majina yao wala kupigwa
picha, wamesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika kijiji cha Idege,
ambapo kwa madai yao walimkamata na vithibitisho ambavyo ni kamba za
kufungia mifugo (ng'ombe na mbuzi)
Wamesema
wamechoshwa na vitendo vya wizi katika kata yao na wilaya kwa ujumla na
kusema kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na madai ya kuiba mifugo ya watu
ambayo ni ng'ombe na mbuzi, katika maeneo ya Tandala, Ibaga, na huko
Idege ambapo ndipo alipokuwa akiishi, hivyo vitendo hivyo vimewachosha
Mwandishi
wa eddy blog alipouliza kama wanauhakika kuwa mtuhumiwa huyo ndiye
mwizi wa mifugo walisema ndiyo, lakini hawakutaka kuithibitisha tuhuma
hiyo, na kusema ili iwe fundisho kwa wengine watawaua watuhumiwa wote wa
wizi watakaowakamata!
"Dawa itakuwa hii, tumechoka kuibiwa, kila mwizi tutakayemkamata dawa itakuwa hii" walisema wananchi hao kwa jazba
Mtandao
huu ulishuhudia wananchi hao wakimpa kipigo cha mbwa mwizi mtuhumiwa
huyo kwa mateke, fimbo, na mawe jambo lililompelekea mtuhumiwa huyo
kufariki dunia baada ya kuvuja damu nyingi
Mtuhumiwa
huyo wakati akiendelea kupigwa kulikuwepo na kamba anazotuhumiwa kuwa
ni za kufungia mifugo anayoiiba, nguo, begi na mablanketi pamoja na unga
Baada
ya taarifa za mauaji hayo kufikishwa kituo cha polisi Makete, polisi
walifika eneo hilo na kuuchukua mwili wa marehemu ambao ulionekana
kujeruhiwa zaidi sehemu ya kichwa, na kusema taarifa zaidi zitatolewa
Endelea
kufuatilia Eddy Blog kupata taarifa ya kipolisi kuhusu mauaji hayo ya
kinyama, kama wapo waliokamatwa kuhusika na tukio hilo na mengine mengi