UTINGO AMUUA UTINGO MWENZAKE KWA KUMGONGA NA LORI

MKAZI wa Temeke, Abdallah Killiah, ambaye ni Utingo, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari la mizigo lililokuwa likiendeshwa na utingo baada ya dereva wake kuliacha na kufuatilia kontena kwenye yadi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea juzi, 11 jioni maeneo ya Vingunguti Relini na kuhusisha gari hilo T 646 ABE ya Scania lenye trailer T 170 AGR.

Alisema gari hilo lilikuwa kwenye foleni  na ndipo utingo wake alipolisogeza  na kumgonga Killiah ambaye ni utingo wa gari jingine la mizigo lenye namba T 177 AQB lenye trailer T 267 BAA na kufariki dunia papo hapo. Maiti imehifadhiwa Hospitali ya Amana.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo