TANROADS IRINGA WAZIDIWA NGUVU NA WAHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Na Martha Magessa-Iringa
WAKALA wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Iringa imekiri kuzidiwa nguvu na waharibifu wa miundombinu ya barabara eneo la Ndiuka barabara kuu ya iringa morogoro, manispaa ya Iringa.

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Iringa, Mhandisi Paulo Lyakurwa ameomba msaada wa jeshi la Polisi katika kukabiliana na waharibifu hao ambao ni madereva wa magari makubwa ya mizigo na vijana waosha magari wanaotumia eneo la maegesho kuosha na kufanya matengenezo ya magari yao.

Amesema maafisa wa Tanroads wamekuwa wakitishiwa na waharibifu hao kila wanapojaribu kuwakamata kwa kukiuka sheria za barabara na wanaofanya matengezo, kuosha au kupata ajali huaribu miundombinu ya barabara na kukiuka sheria ya Barabara Namba 13 ya mwaka 2007 kifungu cha 54 kinachowataka kulipa faini, kama fidia ya kukarabati au kuirejesha kama ilivyokuwa.

Hata hivyo mhandisi Lyakurwa ameongeza kuwa maegesho hayo hayakujengwa kwa ajili ya matengenezo ya magari yao wala kwa ajili ya kuosha magari yao watambue kwamba mafuta ya magari, maji na sabuni vikikaa kwa muda mrefu barabarani vinafifisha ubora wa lami na hatimaye uharibifu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Irinnga kuwatafutia eneo mbadala vijana wanaofanya biashara ya kuosha magari katika eneo hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo