Katika
hali isiyokuwa ya kawaida,Mashabiki wa timu ya Simba wameanza tena
kung'oa viti vya kukalia uwanjani hapa na kuwatupia MashabiKi wenzao wa
Timu ya Yanga waliofurika kwa wingi uwanjani hapa,kwa kile kinachodaiwa
kuwa hawataki kukaa nao sehemu moja.
Picha zote na Othman Michuzi wa MICHUZI MEDIA GROUP.
Picha zote na Othman Michuzi wa MICHUZI MEDIA GROUP.
Mashabiki
wa Timu ya Simba wakiendelea kuwarushia viti Mashabiki wa timu ya Yanga
kabla hata ya mtanange wenyewe kuanza uwanjani hapa.
Viongozi
wa timu ya Yanga wakiwaomba Mashabiki wao kuhama katika eneo hilo na
kwenda kujibana katika eneo walilotengewa kama wana Yanga.
Mashabiki wa timu ya National Al Ahly wakiongea na Askari Polisi kuomba wakalizuie tatizo hilo.
Askari
Polisi wakiongea na Viongozi wa Timu ya Yanga ili waweze kwenda
kuwaomba mashabiki wao waaondoke katika upande ule unaodaiwa kuwa ni wa
Mashabiki wa Simba.
Mambo yalianza kama masihara huku wengine wakitaniana kabisa.