Ukimuuliza mwenyeji yeyote wa Dar es salaam ni
sehemu gani anazozijua wanakaa watu wenye uwezo wa kifedha na hata
baadhi ya viongozi wakubwa wa Serikali, basi lazima atakutajia na
Mikocheni.
Pamoja na hilo, Mikocheni ni moja ya maeneo yanayojaa maji sana
kipindi cha mvua Dar es salaam kama ambavyo unaona kwenye baadhi ya
picha ya juu na hii inayofata hapa chini.
Sehemu nyingine ambazo zipo kwenye hizi picha hapa chini ni pamoja na Kinondoni na Kijitonyama.