MTUMBWI WAZAMA BAHARINI HUKO MTWARA, HABARI KAMILI IPO HAPA

Taarifa kutoka Mtwara ambazo zimethibitishwa na jeshi la Polisi Mtwara ni kuhusu Mtumbwi ambao umezama wakati ukivuka kutoka kitongoji cha Ng’wale kwenda ng’ambo ya pili ambapo ndiyo sehemu waliyokuwa wanashukia abiria waliokuwepo lakini kabla hawajafika upande wa pili mtumbwi huo ulizama.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjd0zkhZ5k2yEP-g5JsJbXuPNXENMQIm89O_-GMpqqvLLUmyDCTf4L8iM3EgArJI9r5EzZQGUUjWI3LMjmOd2fBMQN_4yAZaaXxeYvSTowZ-0Nt0rM2G08xuamtuY_ZRz4AQUTnSpV0OsWf/s1600/DSC_0927.JPG Tayari Watu 21 wamefikishwa katika hospital ya mkoa wa Mtwara kwa matibabu ambao wote ni wakina mama pamoja na mtoto mmoja wa kiume wa mwaka 1,waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni wakina mama 3

Mtumbwi huo unahisiwa ulikuwa na abiria 24 pamoja wahusika wa mtumbwi huo wawili kwa pamoja jumla ya watu waliokua kwenye mtumbwi huo ni 26,wakina mama hao walikua wanatoka kutafuta samaki kwa ajili ya biashara.

Jeshi la polisi bado linamtafuta Dereva wa Mtumbwi huo ambaye inasemekana aliogelea na kutoweka baada ya mtumbwi kuzama

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika ingawa baadhi ya abiria wanadai ni upepo mkali na mvua iliyokuwa inanyesha.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo