MESSI WA SIMBA AVUNJA MLANGO UWANJA WA TAIFA BAADA YA KIPIGO CHA COASTAL UNION


Na Baby Akwitende, Dar es Salaam KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ anadaiwa kuvunja kioo cha mlango wa chumba cha kubadilishia nguo cha timu yake leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mechi dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Wakundu wa Msimbazi wakifungwa 1-0.

Pamoja na ushahidi uliotolewa na wafanyakazi wa Uwanja wa Taifa kwa askari Polisi kwamba, Messi ndiye aliyevunja kioo, hicho lakini wachezaji wenzake na viongozi wa Simba SC walimtetea.

Polisi walishindwa kuchukua hatua yoyote kuhofia kusababisha vurugu na mchezaji huyo aliondoka uwanjani hapo kuelekea kwenye basi la timu yake akisindikizwa na baunsa. 

Tukio hilo limechukuliwa kama hasira za kipigo cha bao 1-0 nyumbani mbele ya Coastal Union katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 
CREDITS:BIN ZUBEIRY


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo