Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa kwa shangwe na Wanachama
mbalimbali wa chama hicho mapema leo asubuhi alipokuwa akiwasili kwenye
ofisi za CCM Wilaya ya Ilala,ambapo alizungumza machache na kamati ya
siasa ya Wilaya na baadae kuanza ziara rasmi wilaya ya Ilala.
Pichani
kulia ni Mwenyekiti Mkoa wa CCM,Dar Es salaam Ndugu Ramadhan Madabida
akizungumza jambo mbele ya kamati ya Siasa ya mkoa (hawapo pichani)
mapema leo,kwenye ofisi Kuu za CCM mkoa,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Abdulrahman Kinana (pichani kushoto) anaanza rasmi ziara ya siku nne
mkoani humo,ambapo atatembelea wilaya ya Ilala (ambayo ameianza
leo),Temeke na Kinondoni. Lengo la ziara hiyo ikiwa ni kuimarisha chama
cha CCM na kuhamasisha na kutenda utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi,sambamba na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Pichani
kulia ni Mwenyekiti Mkoa wa CCM,Dar Es salaam Ndugu Ramadhan Madabida
akimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana taarifa ya hali
ya kisiasa mkoani Dar es salaam,mapema leo mara baada ya kufanyika kikao
kifupi cha kuanza ziara ya siku ya nne mkoani humo
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye kikao kifupi
mbele ya kamati ya Siasa ya mkoa mapema leo,kwenye ofisi Kuu za CCM
mkoa.Ndugu Kinana anaanza rasmi ziara ya siku nne mkoani humo,ambapo
atatembelea wilaya ya Ilala (ambayo ameianza leo),Temeke na Kinondoni.
Lengo la ziara hiyo ikiwa ni kuimarisha chama cha CCM na kuhamasisha na
kutenda utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi,sambamba na ukaguzi wa miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Baadhi
ya Wananchi wakiutazama msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
(haupo pichani),ulipokuwa ukiwasili kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Ilala