Kufuatia
mpango kabambe wa kuelimisha jamii dhidi ya makosa mtandao tayari kumekua na
video za katuni, Mchezo wa komputa “Computer gane”, majarida ya katuni pamoja
na machapisho mengine yote yakiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii juu ya
jinsi ya kujilinda dhidi ya makosa mtandao kuanzia ngazi ya mtu binafsi hadi
kufikia ngazi ya kitaifa.
Picha:
Mfano wa Vijarida vinavyo toa elimu dhidi ya usalama mtandao.
Aidha,
Bwana. Yusuph Kileo ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuangalia kwa
karibu namna itakavyo unganisha nguvu kuhakiki jamii ya watanzania inatambua
kwa kina maswala ya husuyo uhalifu mtandao pamoja ulinzi mtandao. Kileo aeleza
ni vyema maswala yaha ya uhalifu mtandao yanayoshika kasi sana kwa sasa
yanatazamwa kwa karibu ili kuhakiki jamii ya watanzania inabaki salama
kimtandao.
Link:
Mfano wa Video za Katuni zinazotoa elimu ya usalama mtandao.
Athari
za makosa ya kimtandao ni kubwa sana endapo hatua za msingi za kudhibiti
uhalifu mtandao hazitochukuliwa kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi hadi taifa
kwa ujumla. Mataifa makubwa tayari wamesha yaona haya na sasa kumekua na
jitihada mbali mbali zenye malengo ya kukabiliana na uhalifu mtandao.
Kwa
upande mwingine bwana Yusuph kileo ameasa vijana kuwa na juhudi ya kusomea
maswala ya ulinzi mtandao kutokana na uhaba mkubwa ulioko wa wataalamu wa
maswala ya ulinzi mtandao katika ngazi za dunia huku akitolea mfano mataifa
makubwa kuanza kutengeneza majeshi mahususi yatakayokuwa yakikabiliana na vita
mtandao “Cyber war”