Abdulaziz Lindi
Katika Misako inayoendelea Mkoani Lindi, Jeshi la Polisi wilaya ya
Lindi Inawashikiliwa watuhumiwa watatu kwa makosa ya kupatikana na madawa ya kulevya aina ya Heroin pamoja na Miundo mbinu ya Kampuni ya simu kinyume na Sheria.
Katika Misako inayoendelea Mkoani Lindi, Jeshi la Polisi wilaya ya
Lindi Inawashikiliwa watuhumiwa watatu kwa makosa ya kupatikana na madawa ya kulevya aina ya Heroin pamoja na Miundo mbinu ya Kampuni ya simu kinyume na Sheria.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Lindi, Kamishna msaidizi Renatha Mzinga alieleza kuwa kwa Ushirikiano
mkubwa waliopewa na wanajamii wamefanikiwa kumkamata Bw Salum Shaban Mapande(32)Mkazi
wa Dar es sallam akiwa na madawa ya kulevya kete 42 kubwa na ndogo 104
zenye uzito wa Gram 58 na pesa taslim tsh 2,827,500 zinazosadikika kuwa
za mauzo ya madawa hayo.
Watuhumiwa
wengine waliokamatwa ni pamoja na mwanafunzi wa Chuo cha Utalii mjini
Lindi, Masudi Mohamed(19) aliekutwa na kete 35 za bhangi huku Abdul Mahamud na Halfan Salum waliokutwa na nyaya za kampuni ya simu TTCL Zenye Uzito wa kg 5.
Akielezea
matukio hayo, Kamanda Mzinga alisema kuwa Kwa sasa mkoa wa Lindi
umeanza kampeni kubwa ya kupambana na uhalifu mbalimbali ikiwemo
kupambana kuondoa wimbi la uingizaji na uuzaji wa madawa ya kulevya
ambalo kwa sasa kuna ongezeko kubwa la utumiaji na uuzaji wa madawa hayo
ikiwemo pombe haramu (GONGO).
Aidha
Kamanda Mzinga ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kujidhatiti na
kufichua wahalifu wakiwemo wauza madawa ya kulevya ambapo Jeshi lake
litatoa Ushirikiano na Usiri kwa watakaotoa taarifa zinazoashiria
Uvunjifu wa Amani ikiwemo za Usalama barabarani.