Na Magreth Kinabo – Maelezo, Dodoma
BAADHI YA WAJUMBE wa Bunge la Maalum la Katiba wamewataka wajumbe
wenzao kujikita katika mchakato wa mjadala wa Rasimu ya Katiba Mpya
itakayozingatia maslahi ya taifa na kuwanufaisha Watanzania badala
kujitazama mwenyewe.
Kauli hiyo imetolewa leo na mjumbe wa bunge hilo, ambaye ni mmoja wa
kiongozi wa kundi la TANZANIA KWANZA Dk. Emmanuel Nchimbi wakati
akizungumza katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na Shirika la
Utangazaji la Tanzania(TBC), ambapo alisema msingi wa kundi hilo ni
kushiriki katika mchakato huo na kuaichaTanzania ikiwa moja.
“ Tunataka kushiriki katika kumaliza kazi ya Bunge hili na kuaicha Tanzania ya leo na Kesho baada kumaliza ,” alisema Dk. Nchimbi.
Aidha DK . Nchimbi alisema kuwa mchakato huo usiwe sehemu ya
kujipatia madaraka, bali iwe ya kuwaongoza Watanzania katika kuwapatia
maendeleo.
Alisema bado watu wana mahitaji makubwa ya huduma za kijamii kama vile elimu, afya, ufugaji, na miundombinu.
Alisema bado watu wana mahitaji makubwa ya huduma za kijamii kama vile elimu, afya, ufugaji, na miundombinu.
Dk. Nchimbi akifafanua kuhusu suala la kura ya wazi au siri, alisema
bado msimamo wake ni wa kura ya wazi ambao utajenga mfumo wa maadili
ya ukweli na uwazi, huku akihoji kama wanachangia mjadala kwa wazi kwa
nini kura zisipigwe kwa wazi?
Alisema kura ya wazi itasaidia wananchi kutambua michango yao katika maeneo mbalimbali ilivyowakilishwa.
“Tuko hapa kutunga Katiba ya Watanzania mtu atakumbukwa kwa kile alichokisema,” alisisitiza.
Kwa upande wake mjumbe mwingine wa kundi hilo , Charles Mwijage
akingumza katika kipindi hicho aliwataka wajumbe wa Bunge hilo kutumia
njia ya maridhiano pale wanapoona kuna mambo ambayo hajaridhika nayo.
Akizungumzia kuhusu suala la kuwepo kwa Serikali tatu alisema , lina
gharama ya kuuendeshaji kwani ,italazimika kuwa na tume nane kuwa na
mabunge matatu yenye viongozi tofauti ambayo yataongeza gharama
Akizungumza baada ya kuahirishwa wa kikao cha Bunge hilo, mjumbe
kutoka Asasi ya Vijana, Siti Abbas Ali , ambaye pia ni Mwanasheria
kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) aliwataka
Watanzania kuondoa hofu juu ya mchakato huo,hivyo katiba hiyo itakuwa
ni ya Watanzania.
Alisema wataangalia kwa upana haki za vijana, watoto, wanawake na makundi maalum kwa upana.