BUNGE LA KATIBA LAPITISHA KURA YA SIRI NA YA WAZI KUTUMIKA KWA PAMOJA


Wajumbe wa bunge la Katiba mpya wamepitisha kura ya wazi na siri kutumika kwa pamoja katika kuendesha bunge hilo la katiba baada ya majuma kadhaa ya mabishano juu ya utaratibu upi utumike.

Tangu kuanza kwa bunge maalum la katiba kwa zaidi ya siku 40 mgongano mkubwa umekuwa katika kanuni za 37 na 38 kuhusu suala la upigaji wa kura za wazi na siri.

Makubaliano ya kura ya wazi na siri yanaanzia katika upigaji kura wa kuridhia mapendekezo hayo ya kanuni waliotaka kura za siri haya,wa kura za wazi na sawa.

Tayari wajumbe hawa wametumia siku 40 kutunga na kupitisha kanuni za kuweza kusimamia shughuli za uendeshaji wa bunge hili maalum la katiba mjini Dodoma.

Chini ya kamati ya muda ya maridhiano baada ya kukaa kwa masaa kadhaa tangu usiku wa machi 27 kimsingi wamekubaliana kuendelea na mchakato wa utungaji wa katiba mpya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo