Kaimu
Meneja wa Bandari ya Tanga, Freddy Liundi (wa pili kutoka kushoto) akitoa
maelezo juu ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Bandari ya Mwambani kwa kiongozi
wa timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo
kutoka Tume ya Mipango ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia
Kongane ya Sekta za Uzalishaji, Bw. Maduka Kessy.
Timu
ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo, kutoka Tume ya Mipango wakiongozwa na Naibu
Katibu Mtendaji, Bw. Maduka Kessy (wa kwanza kushoto) wakipata maelezo ya
maendeleo ya ujenzi wa bandari ya mwambani ambapo upembuzi yakinifu tayari umeshafanyika.
Kaimu
Meneja wa Bandari ya Tanga akionesha eneo ambapo bandari ya Mwambani itajengwa.
Picha
ikionesha eneo la mwambani ambako ndipo miundombinu ya bandari itajengwa
Timu
ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakisikiliza maelezo
kutoka kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Freddy Liundi (wa pili kulia)
ufukweni mwa bahari, eneo ambapo bandari ya Mwambani itajengwa.
Picha na Joyce Mkinga