“Nyimbo zipo lakini sija release nyimbo…sijatoa nyimbo so far na sijui nani ameimba na sijawahi hata kuisikia” Alisema Alikiba alipozungumza na mtangazaji Renatus Kiluvya kupitia New Chapter ya Radio Free Africa.
“Sijawahi kuisikia na sitaki kutoa comment yoyote kwasababu navyojijua mimi first of all najikubali sana, la pili watu wananiambia niko unique afu surprise watu wananiambia nimetoa nyimbo sijui tumesikia nyimbo inaitwa Rosa yaani hiyo sijaelewa bado.” Alisema hit maker wa Cinderella.
Aliongeza kuwa kuna uwezekano kuwa kuna watu wamefanya makusudi kufake wimbo huo uonekane ni wake kutokana na ukimya wake, au wamefanya sayansi sauti isikike kama yake, au huyo aliyeimba ni role model wake ndio sababu kaamua kufanya hivyo.
“Wameona nimekaa kimya sana wakaona ngoja watoe nyimbo na wakatumia jina la Alikiba, it doesn’t make sense kama unatoa nyimbo unategemea kutoka kwa jina la mtu flani, I think ni trick moja ambayo imefanywa sielewi na nani lakini I don’t know if in a good way or bad way.”
Pia Ali K alizungumzia ujio wake mpya,
“Ujio wangu uko very soon, sasa hivi wakae tayari fans wangu na kilichonifanya nikae kimya kingi watajua ni kitu gani na watani understand kabisa maana ya kukaa kimya.”Msikilize hapa