Mstahiki
meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akifungua
kikao kwa maombi katika baraza la madiwani lilofanyika mwishoni mwa wiki
kushoto ni naibu meya Gervas Ndaki na kulia Mkurugenz Theresia Mahongo
kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa. (picha
na Denis Mlowe).
Juu
na chini ni Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakiwa katika
kikao cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri mwishoni
mwa wiki.
Habari na picha na Denis Mlowe.
MIONGONI
mwa watu 6003 mkoani hapa waliopima afya zao kwa hiyari katika kipindi
cha Oktoba hadi Disemba mwaka jana, watu 379 wamebainika kuwa na
maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).
Akizungumza
katika kikao cha utekelezaji wa shughuli za ukimwi zilizotekelezwa na
Kamati ya Kudhibiti Ukimwi mbele ya baraza la madiwani kwa kipindi cha
robo ya pili Oktoba na Disemba mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa kamati
hiyo, Naibu Meya Gervas Ndaki, alisema kati ya waliojitokeza kupima na
kupata ushauri nasaha, wanaume walikuwa 3074 wanawake 2,929.
Ndaki alisema kati ya watu 379 waliopima kwa hiari na kukutwa na maambukizi,146 ni wanaume na wanawake ni 233. Alisema
huduma ya kuzuia maambukizi ya vvu/ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto, wajawazito 1,287 walijitokeza na kupata ushauri wa nasaha na kati
yao, 84 sawa na asilimia 6.5 walikutwa na maambukizi.
Ndaki
alisema mapambano ya ukimwi yanaambatana na huduma za tiba sahihi ya
magonjwa ya ngono na jumla ya watu 361, wanaume 110 na wanawake 251,
walipata tiba sahihi ya magonjwa ya ngono.
“Maambukizi
ya ugonjwa wa ukimwi yanaendelea kuwepo na tunajitahidi sana
kuwahamasisha wananchi kujitambua na kutumia sana kondom na pia
tumefanya sana kampeni kwa wananchi wanaotakiwa kwenda tohara kujitokeza
kwenda katika hospitali na vituo vya afya vinavyotambulika kutoa huduma
ya tohara” alisema Ndaki.
Aliongoza
kuwa huduma ya kitabibu ya tohara kwa wanaume ilitolewa kwa jumla ya
wanaume 171 walitahiriwa na kati ya waliopima vvu wanaume 160 na hakuna
aliyekutwa na maambukizi.
Kwa
upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani
Mwamwindi aliwataka watendaji kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya
maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa kuwasisitiza wananchi kwa
kuwapa elimu kuondokana na maambukizi mapya.
alisema mkoa wa Iringa una nafasi kubwa sana wa kuwa wa mwisho kama kila
mmoja atatumia nafasi yake kuelimisha vijana kwa wazee katika mapambano
dhidi ya ukimwi.