Mkurugenzi
wa mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu.
Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda umeeleza kusikitishwa na taarifa za
blog ya Rwanda “News of Rwanda” ambayo inaunga mkono serikali ya nchi
hiyo iliyotolewa mwishoni mwa juma zikimtuhumu rais wa Tanzania Jakaya
Kikwete kwa kuunga mkono na kufanya mikutano na wanachama wa makundi ya
waasi yanayopingana na serikali ya Rwanda.

Akizungumza
na Sauti ya Amerika mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania
Salva Rweyemamu amesema wao wameshangazwa kwa sababu mwaka jana
kulikuwa na matatizo na marais wa nchi hizo wameshazungumza vizuri
wakakubaliana na kuonyesha kwamba sasa mambo yameisha na kwamba
wanaendeleza urafiki wao, udugu wao na ujirani mwema wa miaka mingi kati
yao na kuongeza kwamba hilo ni jambo la kusikitisha sana kwa upande wa
Tanzania.
Ametoa
wito kwa vyombo vya habari nchini humo visaidie kujenga uhusiano mwema
na visiwe mwanzo wa choko choko ya kugombanisha watu akiuliza kuwa
“Tanzania wakigombana na Rwanda magazeti yatauzwa?” au mkiwa kwenye hali
ya vurugu kama ilivyo nchi zingine ambapo watu wanapigana kila siku
kuna watu wananunua magazeti pale?
Kusikiliza mahojiano ya Salva Rweyemamu na VOA bofya hapa.
http://www.voaswahili.com/content/article/1841294.html