BREAKING NEWS: MTANGAZAJI WA EAST AFRICA RADIO AKUTWA AMEKUFA NDANI MWAKE

Marehemu Kenneth Kidago Lyanga enzi ya uhai wake.


Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha East Africa aliyekuwa akifanya kipindi cha 5 sports, Kenneth Kidago amefariki dunia.

Taarifa ambazo pia zimethibitishwa na mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho zinaeleza kuwa tangu jana januari 30,2014 Ken hakuonekana kazini ambapo simu zake zilikuwa zikipigwa bila majibu ikabidi uongozi wa EATV kutoa taarifa kwa jeshi la polisi nchini Tanzania,walipofika nyumbani kwake Mlalakua jijini Dar es salaam wakagonga mlango hakufungua kabidi wavunje na kuingia 
 
Taarifa zinadai kuwa Kenneth amekutwa amefariki akiwa amekaa kwenye kochi wakati akiangalia televisheni kwa kuwa televisheni hiyo imekutwa ikiendelea kuonesha vipindi
 
Taarifa zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa sababu ya kifo chake.

Ken Kidago aliwahi kuwa mtangazaji wa Radio Ukweli ya mjini Morogoro kabla ya kwenda Arusha ambapo alirejea jijini Dar es salaam hivi karibuni na kujiunga na East Africa Television

Mipango ya mazishi ya Kenneth Lyanga inafanywa na familia yake. 

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Kenneth Kidago Lyanga Mahala Pema Peponi, Amina.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo