SHABIKI WA ARSENAL AMUUA WA LIVERPOOL KWA KUMCHOMA KISU WAKATI WAKITAZAMA MECHI

Olivier Giroud
Straika wa Arsenal Olivier Giroud wakati wa mechi yao dhidi ya Liverpool uwanjani Anfield Februari 8, 2014. Picha/AFP
======
MWANAUME mmoja alidungwa kisu hadi kufa wakati akitazama mechi ya kandanda mjini Meru kenya baada ya kutofautiana na mwenzake kuhusu mechi iliyokuwa ikiendelea.
Marehemu alikuwa akitazama mchuano kati ya timu ya Arsenal na Liverpool wakati walipoanza vita katika baa ya Marete eneo la Makutano.

Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa Polisi eneo hilo Tom Odero alisema mshukiwa David Mwangi, ambaye ni shabiki wa timu ya Arsenal alimdunga kisu Anthony Muteithia, shabiki wa Liverpool. 

Bw Odero alisema mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 25 alikufa alipokuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Meru.

“Mshukiwa alilazimika kutoroka lakini wakazi walifanikiwa kupata pikipiki aliyokuwa nayo na kuiwasilisha kwa maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Meru. Msako wa kumkamata umeanzishwa,”alisema Bw Odero.

Mkuu huyo wa polisi alisema uchunguzi umeanzishwa kutambua chanzo cha mzozo wa wawili hao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo