BUNGE LA UGANDA LAPITISHA MUSWADA WA KUWAFUNGA JELA MAISHA MASHOGA NA WASAGAJI NCHINI HUMO

Bunge la Uganda Ijumaa lilipitisha mswada ambao utafanya baadhi ya vitendo vya ngono kati ya watu wa jinsia moja kupewa adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Mswada huo awali ulishtumiwa na  makundi ya kutetea haki pamoja na serikali za Magharibi ikiwemo Marekani kwa sababu ulijumuisha adhabu ya kifo.
 
 Mswada uliopitishwa Ijumaa unatoa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa yeyote atakayehukumiwa kwa kile ilichosema ni “vitendo vilivyopita mipaka” vya ngono kati ya watu wa jinsia moja.
Waziri Mkuu Amama Mbabazi alikaririwa akisema kuwa serikali ya Uganda itafanya mashauriano zaidi kuhusu mswada huo ambao unahitaji kutiwa saini na Rais Yoweri Museveni kabla ya kuwa sheria kamili nchini humo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo