Amesema umefika wakati kwa viongozi hao kutumia imani hiyo ya kusikilizwa na wananchi kupata suluhu la migogoro ya ardhi pamoja na kuondoa matabaka baina ya wafugaji na wakulima yaliyosababishwa na migogoro hiyo.
Ni katika Uzinduzi wa Jukwaa la Ardhi Tanzania ndipo Waziri Pinda anasema jitihada za ziada zinahitajika kutoka kwa viongozi hao kutatua migogoro hiyo ya ardhi.
Ameongeza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana zaidi kulinda amani kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi.
Kwa Upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania KKKT Dk. Alex Malasusa anasema kuna haja ya kuweka mipango mizuri ya usimamizi wa ardhi kutokana na idadi ya watu wenye mahitaji ya ardhi kuongezeka kila siku.
Jukwaa la Ardhi Tanzania limeshirikisha viongozi wa dini ya Kiislamu na kikristo, serikali, asasi za kiraia na wadau mbalimbali ambapo miongoni mwa majukumu yake ni kutafuta suluhu la migogoro ya ardhi nchini kupitia ushirikishwaji wa jamii husika kufanya maamuzi yenye lengo la kudumisha amani ya nchi.