MOTO WATEKETEZA BWENI LA WAVULANA NJOMBE SEKONDARI JANA JIONI


 Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Njombe Kimepongezwa Kwa Kuwahi Kufika Eneo la Tukio na Kufanikisha Kuzima Moto Huo
 Wanafunzi Wakihamisha Baadhi ya Vitu Vilivyookolewa Katika Bweni Hilo
 Kiongozi wa Bweni Hilo Akizungumzia Jinsi Moto Ulivyotokea.



Na Gabriel  Kilamlya Njombe

Katika Hali Isiyo ya Kawaida Moto Mkubwa Umeunguza Bweni la Wanafunzi Katika Shule Ya Sekondari Njombe [NJOSS] na Kuteketeza Vitu Mbalimbali Vya Wanafunzi Hao Jioni ya jana.

Tukio Hilo Limetokea  Majira ya Saa Kumi na Mbili Jioni Ambapo  Vitu Mbalimbali Ambavyo ni Vifaa Vya Masomo Kwa Wanafunzi Hao Vimeteketea Kwa Moto Huo.

Wakizungumza na mtandao huu Katika Eneo la Tukio Baadhi ya Wanafunzi wa Shule Hiyo Wamesema Bado Hawajatambua Chanzo cha Moto Huo Japo Kwa Taarifa za Awali Zinaeleza Kuwa ni Shoti ya Umeme.

Akizungumzia Tukio Hilo Kiongozi wa Bweni Katika Shule Hiyo ya Wavulana  Amesema Kuwa Moto Huo Umetokea Wakati Wanafunzi Wakiwa Ukumbini Kuangali Mpira Kwenye Luninga.

Akizungumzia Tukio Hilo Diwani wa Kata ya Mjimwema Bwana Jimy Ngumbuke Amesema Kuwa Pamoja na Kutokea Kwa Athari Kubwa Kwa Wanafunzi Hao
Lakini Hakuna Mwanafunzi Aliyejeruhiwa Wala Kupoteza Maisha.

Bwana Ngumbuke Pia Amepongeza Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Njombe Kwa Kuwahi Kufika Katika Eneo la Tukio na Kufanikiwa Kuzima Moto Huo Licha ya Kuunguza Baadhi ya Mali za Wanafunzi.

Bado Thamani Halisi ya Hasara Iliyotokea Kufuatia Kutokea Kwa Moto Huo Huku Serikali Ikiahidi Kuendelea Kutoa Taarifa Zaidi ya Hali ya Tukio Hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo