Mkuu
wa mkoa wa Iringa, Dr. Christina Ishengoma leo amezungumza na wafanya
biashara wa manispaa ya Iringa katika ukumbi wa community centre uliopo
eneo la Kitanzini katika manispaa ya Iringa, mada kuu ilikuwa inahusu
mgomo wa wafanya biashara kupinga mashine mpya za kutoa risiti
zilizotolewa na TRA ili zitumike katika biashara zao.
baadhi ya wafanya biashara walio hudhuria katika mkutano huo uliofanyika leo.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Iringa,Bw. Lucas Mwakabunge, akizungumza na wafanya biashara katika mkutano huo.
Pichani ni baadhi ya Wafanyabiashara wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa katika mkutano huo.
Mkuu
wa mkoa huyo alisisitiza kuwa elimu inatakiwa kutolewa kwa wafanya
biashara hao kuhusu umuhimu wa mashine hizo kwa kuwa wafanya biashara
wengi wameonesha hali ya kutoridhishwa nazo na hata kufanya maandamano
ya nchi nzima wakipinga matumizi ya mashine hizo na kutaka kendelea
kutumia mfumo wao wa zamani wa kutumia vitabu.
Mkuu
wa mkoa huyo alidai kuwa yeye sio muhusika mkuu wa suala hilo lakini
kama ilivyo, ni wajibu wake kuzungumza na hata kuwasaidia watu wake
hivyo aliwataka wafanya biashara hao fungua maduka kwani kilio chao
kimesikika na serikali inalifanyia kazi suala hilo.
PICHA ZAIDI INGIA MJENGWA BLOG.