Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ltd, wachapishaji wa magazeti ya
Mtanzania, Rai, Bingwa, Dimba na The African, Absalom Kibanda,
akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni hiyo, hawapo pichani katika hafla
fupi ya kumpongeza ushindi wake katika kesi iliyokuwa inamkabili
iliyodaiwa kuwa ni uchochezi juzi. Halfa hiyo ilifanyika katika ofisi za
Kampuni hiyo, Sinza Kijiweni.
Absalom Kibanda kushoto akifurahia jambo kutoka kwa MC, Sidi Mgumia,
ambaye ni mwandishi wa Gazeti la The African. Kulia kwa Sidi ni Ofisa
Mtendaji Mkuu wa New Habari, Hussein Bashe.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo, Hassan Bumbuli, Jonathan Tito,
Kambi Mbwana, Grace Hoka na Mareges Paul wote wamesimama. Ilikuwa
burudani kubwa, huku wakiangalia kinachojiri katika tukio hilo la aina
yake katika hafla hiyo.
Shughuli inaendelea hapa. Kila mmoja macho mbelee. Hongera bwana Abasalom Kibanda..
Weee madada wa New Habari hawa, Jenifer Ullembo kushoto na Zaituni Kibwana. Wote walikuwapo na kushuhudia kinachoendelea.
Muda wa burudani ukafika, Kwaito kwa kwenda mbele.
Ukitaka umuudhi Mwani Nyangassa, Mhariri wa Michezo wa Gazeti la
Mtanzania, kitu white hicho basi mnyime muziki. Atakutoa ndukiiiiiiiiii.
Nyuma ya Mwani Nyangassa ni Esther Mbusi. Mwenye miwani ni baba
shughuli, Absaol Kibanda, naye akionyesha ubora wake.....
MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA HAFLA YA KUMPONGEZA ABSALOM KIBANDA KWA KUSHINDA KESI
By
Edmo Online
at
Sunday, February 02, 2014