KUFURU: POSHO YA WAJUMBE BUNGE LA KATIBA NI SH. 700,000/= KWA SIKU!

Posho kwa siku kwa kila mjumbe wa Bunge la Katiba ni sh 700,000 kwa siku kwa muda wa siku 70 maana yake ni kuwa kila mjumbe atalipwa milioni 49!

Aidha, sheria inawaruhusu kuongeza siku nyingine 20 na kufanya jumla ya siku 90. Kitendo hicho kitapelekea kila mjumbe kujipatia kitita cha Sh. milioni 63.

Inadaiwa kiasi hicho cha posho kilipendekezwa kwa wajumbe hao kwa vile hawana mishahara, wala magari na nyumba kama ilivyokuwa kwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba au wabunge ambao wana mishahara, posho, mafuta ya magari na mikopo!

CHANZO: Tanzania Daima


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo