Na Mwandishi Wetu
MAANDIKO yanasema ‘usitamani mali ya mtu mwigine’!
Ni kweli kabisa, onyo hilo lilichukua fursa yake kufuatia njemba mmoja
aliyejulikana kwa jina la Anton John Mwaweje kunaswa laivu gesti na mke
wa rafiki yake aliyefahamika kwa jina moja la Chalz.
Tukio hilo lilijiri mwanzoni mwa wiki hii kwenye gesti moja maarufu (jina tunalo) iliyopo Buguruni- Malapa jijini Dar es Salaam.
Katika sakata hilo ilidaiwa kuwa, Mwaweje alikuwa akiifahamu vyema
familia ya Chalz sambamba na mke wake (jina lipo) lakini hilo hakulijali
na kumtokia mke wa Chalz ambaye kwa utamaduni wa Kiafrika ni shemejiye.
Habari zikazidi kudai kwamba, ilifika mahali katika kumtaka shemejiye
huyo ambaye alikuwa akimkatalia katakata, Mwaweje alitumia gia nyingine
ikiwemo ya kumuahidi mambo manono kama angekubali kuivunja amri ya 6 ya
Muumba na yeye.
Chanzo cha habari kiliendelea kudai kuwa, ‘Mungu si Athuman wa
Lucas’ siku isiyo na jina jamaa alimtumia ujumbe (SMS) mke wa mwenzake
kwa kutumia maneno ya kumtoa nyoka pangoni kumbe muda huo bwana simu
alikuwa nayo mwenye mke.
Chalz alimwita mkewe na kumuuliza ni nani aliyemtumia ujumbe huo? Ndipo mke akaanika ukweli akisema:
“Mume wangu, wala usikonde. Aliyetuma ujumbe huo si mwingine, ni Anton…”
Mume: “(akihamaki) Anton huyuhuyu?”
Mke: “Huyuhuyu mume wangu. Amekuwa akinitaka kimapenzi kwa muda mrefu sana, namkatalia lakini hasikii.”
Za mwizi 40: Bwana Anton John akiwa na pingu mkononi baada ya kunaswa na kamanda wa OFM pamoja na wanausalama.
Pia, mwanamke huyo alimwonesha mumewe meseji kibao ambazo jamaa huyo amekuwa akimtumia na zile ambazo yeye amekuwa akimkatalia.
“Sasa sikia, mkubalie,” mwanaume huyo alimwambia mke wake huku midomo ikimcheza kwa hasira.
Chini ya usimamizi wa mumewe, mwanamke huyo aliwasiliana na Anton na kumwambia alikuwa na nafasi wanaweza kukutana kwa ajili ya kumsaliti Chalz.
Baada
ya kupanga mipango ya kukutana, mume huyo alipiga simu Global
Publishers kwenye kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kuomba
msaada wa fumanizi ambapo alibahatika kukuta kuna kamera mpya zimewasi
tayari kwa kazi kama hizo.
Baada ya kupata maelezo ya Chalz, OFM ilishirikiana na Jeshi la
Polisi Buguruni –Kwamnyamani jijini Dar na kuandaa mtego ambapo Jumatatu
iliyopita, saa nane na ushee mchana, Anton ambaye naye inasemekana ana
mke aliuingia mtego na kunasa kwenye chumba namba 5 akiwa na mke mwema
huyo.
Ndani ya chumba hicho, Anton alikutwa na boksa tayari kwa mlo wa
wizi ambao alibakia kuendelea kusikia njaa. Mezani, kulikuwa na chipsi
kuku na pombe ambazo zingewapa stimu kabla ya mchezo.
Kitendo cha Chalz kumnasa jamaa huyo na mkewe kitandani kilimpandisha
munkari ambapo nusura afanye ndivyo sivyo lakini alitulizwa na polisi
waliokuwa eneo hilo kwa ajili kulinda usalama.
Kilichofuata baada ya hapo, mgoni huyo akiwa na pingu mkononi
alipelekwa kwenye kituo hicho cha polisi ambapo awali, Chalz alitoa
ripoti ya malalamiko baada ya kugundua jamaa huyo anataka kumtumbukiza
mkewe kwenye mstari wa usaliti.
Mpaka OFM wanaondoka kituoni hapo, taratibu za kisheria kuhusiana na
kesi hiyo zilikuwa zikiendelea huku mgoni huyo akiwa chini ya ulinzi
mkali.
CHANZO: GPL