Ufafanuzi huo umetolewa na Afisa elimu sekondari wilaya ya Makete Mwl. Jacob Meena wakati akizungumza na mtandao huu uliotaka kufahamu sababu za kutokamilika kwa usajili ya sekondari ya kata ya Isapulano kama ambavyo imekuwa ikilalamikiwa na wakazi wa kata hiyo
Mwl. Meena amesema ni kweli mchakato wa kuisajili shule hiyo unaendelea hivyo wananchi wanapashwa kuwa na subira kwa kuwa hatua za usajili zinafuatwa ngazi kwa ngazi na wakati mwingine huchukua muda mrefu hivyo wananchi wasione kama suala hilo limepuuzwa bali linaendelea kufanyiwa kazi hadi hivi sasa
Amesema tayari walishafika wakaguzi kuikagua shule hiyo na kutoa mapendekezo ambayo yanatakiwa kukalimishwa ikiwemo suala la ujenzi wa maabara kwani ni agizo lililotolewa na rais Jakaya Kikwete kuwa shule zote za sekondari nchini lazima ziwe na maabara ifikapo Novemba mwaka huu
Ameongeza kuwa hicho ni kigezo kimojawapo ambacho wakaguzi hao watakapouja tena mwezi ujao kuja kuikagua shule hiyo na kukuta haina maabara hawawezi kutoa usajili hivyo kuwaomba wananchi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha shule hiyo inakuwa na maabara