Na Ibrahim
Yassin,Kyela
WANAFUNZI 292
waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza wilayani Kyela mkoani
Mbeya hawajaripoti shuleni kuanza masomo kutokana na matatizo mbalimbali
zikiwamo ya kupata ujauzito kwa wanafunzi wa kike.
Kauli hiyo ilitolewa
jana na mkuu wa Wilaya hiyo Magret Malenga wakati akipokea msaada wa vitanda 20
vyenye thamani ya million tatu vilivyotolewa na kampuni inayojishughurisha na
ununuzi wa zao la kakao ya Olam Tanzania Limited kwa ajili ya bweni la
wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari ya kata ya Busale iliyopo Stamiko
Kiwira Cor mine (KCM).
Mkuu huyo wa
wilaya alisema kuwa mwaka jana wanafunzi hao hawakuripoti kuanza masomo na wao
kama Serikali watafanya msako wa nyumba hadi nyumba ili kuwabaini
waliosababisha wanafunzi hao wasiripoti shuleni ikiwemo ya kuwachukulia hatua
wale waliowapa ujuzito watoto hao kwa lengo la kuthibiti hali hiyo isitokee
tena.
Aliongeza
kuwa wilaya ya Kyela bado inachangamoto kubwa katika ufauru kwa wanafunzi na
kuwa kwa kuliona hilo Serikali kwa kushirikiana na waau wameamua kujenga
mabweni ili kuwapa urahisi wanafunzi kuweza kusoma kwa ufanisi zaidi na
kupunguza vishawishi wanavyovipata mitaani.
Diwani wa
kata hiyo Ezekia Msyani mbali na kuipongeza kampuni hiyo kwa kuwapatia msaada
huo pia aliwataka viongozi wa bodi kuitisha kikao cha pamoja na wazazi wa
anafunzi ili kupanga namna ya kuweza kukamirisha taratibu na namna ya
kuwawezesha wanafunzi hao kuanza kulala kwenye bweni hilo na kuwa ifikapo
tarehe 30 mwezi wa pili watoto wawe wameanza kulala katika bweni hilo.
Mkuu wa
shule hiyo Juma Kaniki alisema yeye kwa kushirikiana na waalimu wenzake
watahakikisha wanawalinda wanafunzi hao ili wazingatie masomo yatakayopelekea
kuongeza ufaulu na kuwa wanafunzi watapata chakula cha mchana na gharama za
hostel ni 30,000 kwa mwaka na 120 000 kwa ajili ya chakula na hivi sasa
wanajenga uzio ili kudhibit utolo kwa wanafunzi hao.
Mch,Benedictor
Mwansasu mkazi wa kijiji hicho aliitaja changamoto inayopelekea wanafunzi wa
kike kuolewa na wakiume kujishughurisha na vibarua huku wakiacha shule ni
kutokana na waalimu wa shule hiyo
kupenda kuwachapa viboko mara kwa mara wanafunzi hao ambao uamua kuacha shule
na kujiingiza katika vitendo hivyo ambavyo vinachangia kushusha elimu wilayani
hapa.
Akizungumza kwa
niaba ya wanafunzi wenzake Gedtrida Fabian alisema kuwa kitendo cha kampuni
hiyo kuwapatia msaada huo wa vitanda utawapa hueni ya kupata vishawishi mitaani
na kuwa watajikita na kusoma kwa bidii ili kuifanya kampuni hiyo ipate nguvu
tena ya kuweza kuwasaidia pindi watakapohitaji msaada mungine.
Meneja wa
kampuni hiyo Godfrey Okungu kwa upande wake alisema kampuni hiyo imetoa sehemu
ya faida inayoipata katika kuuza zao hilo kusaidia vitanda hivyo kwa lengo la kupunguza changamoto zilizopo mashuleni na
kuwa wataendelea kusaidia pale watakapo ombwa kufanya hivyo.
