UTOROROSHAJI WA MADINI WAISABABISHIA SERIKALI KUPATA HASARA YA MILIONI 547.15

Wakala wa madini nchini TMAA imesema serikali imepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 547.15 zilizosababishwa na utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi kupitia viwanja vya ndege vya Dar Es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka 2013. 

Kadhalika serikali imeendelea kupata hasara ya shilingi bilioni 2 kutokana na kesi 32 kupelekwa mahakamani kwa mwaka 2013 pekee. 

Kutokana na ukaguzi uliofanywa na Taasisi mbalimbali za Serikali imebainika kuwa maeneo ya mipakani na sekta ya usafirishaji ndiko kwenye uhalifu mkubwa wa utoroshaji wa madini hatua inayoifanya Wakala wa Madini Tanzania TMAA kuiomba Serikali kuzidisha nguvu zaidi katika maeneo hayo. 

Ingawa TMAA imekuwa ikifanya jitihada za kudhibiti utoroshaji wa madini hayo, imebainika kuwa wanaofanya uhalifu huo ni Watanzania na Raia wa Kigeni na kwamba changamoto kubwa ni kutoroka kwa wahalifu hao wakiwa katika vyombo vya usalama. 

Kufuatia hali hiyo Wakala hao wakatoa onyo dhidi ya wanaofanya uhalifu wa utoroshaji madini hayo na kuwataka Watanzania kutosita kutoa taarifa kwa vyombo husika. 

Tangu kuundwa kwa Wakala wa Madini Tanzania Mwaka 2012 kesi 37 zimeripotiwa Mahakamani zilizotokana na uhalifu huo ambazo kwa asilimia kubwa zimekuwa zikitokea kwenye viwanja vya Ndege


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo