Naambiwa hii picha ni wakati alipookolewa mmoja wa watu waliorushwa kwenye maji kutokana na dhuruba iliyoipata boti hiyo.
Leo saa tano asubuhi taarifa zilianza kusambaa kuhusu boti ya
Kilimanjaro II ikitokea Pemba kwenda Unguja kupata dhoruba ya kupigwa na
upepo mkali ilipofika kwenye eneo hatari la Nungwi kulikopelekea sehemu
ya mbele ya boti hiyo kuzama kwa dakika kadhaa na kuibuka juu tena.
Kitendo hicho kilipelekea watu ambao idadi yao haijulikani, kurushwa
kwenye maji kwa sababu walikua wamekaa na wengine wamelala kwenye hii
sehemu ambayo ndio ilizama kwenye maji.
Tayari mashuhuda na baadhi ya abiria waliokuwemo ndani wameanza kutoa
ushuhuda wa vifo na majeruhi ambao waliweza kuogelea au kuokolewa
kwenye ajali hii.
Suleiman Masoud ambae yuko msibani Zanzibar kwa sasa, amethibitisha
ndugu zake watatu ambao ni watoto wa shangazi yake wamepotea saa kadhaa
tu baada ya kutoka Pemba safarini kuelekea Unguja wakiwa na hiyo boti.
Anasema ‘katika waliokwenda kutambua miili kaka mtu pia alikuepo
ambapo baada ya kuona maiti ya mdogo wake amezimia mpaka sasa, watoto wa
Shangazi ni watatu wamepotea’
Suleiman Masoud akiwa msibani Mwanakwerekwe Zanzibar leo baada ya kupata taarifa za watoto watatu wa shangazi yake kupotea.
‘Jinsi ilivyotokea kwa watoto hawa watatu, walikabidhiwa kwa mama
mmoja Pemba ili awatizame kwenye meli ambapo kabla ya boti kufika Nungwi
ndani ya boti joto lilizidi hivyo mmoja akawa kapakatwa na huyu mama na
wawili ndio wakatoka nje kwenda kupunga upepo ndio wakakutana na hiyo
dhoruba wakazolewa na hakuwaona tena kuanzia hapo’
Wakati naipandisha hii stori Suleiman ameniandikia msg inayosema
‘mwili wa mtoto wa pili kati ya watatu waliopotea, umeonekana pia’
Unaweza kumsikiliza Selemani hapa chini Kutoka kwenye website ya millardayo.com