Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei amemtaka Zitto aunde chama chake
au atafute kingine cha kujiunga nacho kwa kuwa kwa sasa hana nafasi.
Pia ameshauri kuwa kama ana ndoto za kuwania urais
ni vizuri akatafute vyama vingine kama CCM au CUF kwa kuwa ndani ya
Chadema kwa sasa hahitajiki.
Mtei alisema kuwa kama anataka kubakia na
uanachama wa Mahakama wao hawana shida... “Lakini huwezi kuwapeleka
viongozi wako kortini na bado ukaendelea kubaki kuwa mwanachama wetu.”
Alimtuhumu kwa kuwagonganisha viongozi mbalimbali
ndani ya Chadema na hata kuzua mitafaruku ya hapa na pale huku akisema
kwamba uamuzi wa Kamati Kuu ndiyo wa mwisho.
>>Habari hii imenukuliwa toka ukurasa wa nne wa gazeti la Mwananchi.
>>Habari hii imenukuliwa toka ukurasa wa nne wa gazeti la Mwananchi.
