Mtu
mmoja aliyejulikana kwa jina la Mihayo Mhuri (12) Mkazi wa Center
Maria Kata ya Kakese Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi amefariki
dunia baada ya kuzama kwenye maji ya mto wakati akiwa akiogelea
kwenye maji akichunga ng’ombe.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tano na nusu asubuhi katika
mto wa Katuma Wilayani Mpanda.
Siku
hiyo ya tukio marehemu akiwa na mdogo wake aitwaye Wakasoro Nhuri 7
waliondoka nyumbani kwao na kuelekea kuchunga ng’ombe katika maeneo
ya Karibu na mto Katuma.
Wakiwa
maeneo hayo marehemu alipatwa na jasho na ndipo alipoamua kuvua
nguo na kuingia ndani ya mto Katuma kwa ajili ya kuogelea na
kumwacha mdogo wake akiwa kando ya Mto.
Kamanda
Kidavashari alisema wakati marehemu akiendelea kuoga alizidiwa na
maji na kuanza kuzama chini ya maji ya mto huo kitendo ambacho
kilimshitua mdogo wake ambae alikuwa kando ya mto huo.
Mdogo
wake alianza kupiga kelele za kuomba msaada kwa watu huku akilia
na watu walikusanyika katika eneo hilo na mdogo wa marehemu aliwaeleza
kuwa kaka yake amezama kwenye maji ya mto huo wa Katuma.
Kidavashari
alieleza watu hao walianza jitihada za kumtafuta marehemu baada ya
kitambo kidogo waliweza kuupata mwili wa marehemu ukiwa umekwama
kwenye Gogo pembeni ya mto huku akiwa ameshafariki dunia.
Na Walter M guluchuma
Katavi yetu blog