MAINDA NA THEA WAMEAMUA KUMPOKEA 'BWANA'

Salome Ndumbagwe Mesayo ‘Thea’.
WASANII wa filamu, Ruth Suka ‘Mainda’ na Salome Ndumbagwe Mesayo ‘Thea’ sasa wameonekana kujikita zaidi kwenye mafunzo ya kiroho baada ya hivi karibuni kunaswa kwenye kongamano la ukombozi ndani ya Ukumbi wa Vatican City Sinza jijini Dar walipokwenda kuabudu.
Ruth Suka ‘Mainda’.
Wawili hao walinaswa wakiwa na nyuso za unyenyekevu huku wakionekana kudhamiria kumrudia Mungu na walipoulizwa walisema walikuwa katika kongamano hilo la mafunzo ya kiroho na Biblia kwa siku tatu.
 
 “Sisi tumempokea Yesu, tunawasihi wasanii wenzetu waachane na ushirikina waje huku ambako kuna njia salama, hili ni kongamano ambalo lina mafunzo mema na lina uwezo wa kumbadili mtu kutoka kwenye roho ya kishetani na kuwa na roho safi,” alisema Thea....


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo