FARAJA KOTA AFUNGUKA JUU YA MAPENZI YAKE NA MUMEWE AMBAYE NI WAZIRI..!!

MISS Tanzania 2004, Faraja Kota amefunguka kuwa kamwe hawezi kuingilia kazi za mumewe ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwani anaamini mumewe ana akili nyingi kuliko yeye.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
 
Akizungumza na paparazi wetu, Faraja alisema siyo rahisi kuingilia kazi za mume wake zaidi ya kuzungumza naye kidogo sana kama kuna kitu amekiona anaweza kumshauri kwa sehemu fulani lakini siyo kwa kiasi kikubwa sana.
Faraja Kota.
“Unajua mume wangu ana akili zaidi kuliko hata mimi, naweza kumshauri kidogo tu kama nitakiona kitu fulani na siyo vyote kwa sababu ninaporudi nyumbani anakuwa ni baba zaidi na siyo kama waziri,” alisema Faraja.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo