Na Issa Mnally
NYOTA aliyetamba katika muziki wa kizazi kipya enzi hizo akiwa na Kundi la Daz Nundaz, Ferooz Mrisho, juzikati alikamatwa na polisi na kutupwa lupango katika Kituo Kidogo cha Mabatini, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, baada ya kukutwa akivuta bangi pamoja na vijana wenzake kadhaa maeneo ya Sinza, karibu na Baa ya Meeda.

Habari zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda na baadaye kuthibitishwa
na gazeti hili, zilisema Ferooz alikuwa akivuta bangi katika eneo hilo
kabla ya majirani wanaokerwa na tabia hiyo, kupiga simu polisi wakitaka
kukomeshwa kwa jambo hilo.
“Hapana tumechoka na tabia zao, kila ukipita hapa unakula ‘marashi’
ya bangi tu, vilevile sisi tuna vijana wa rika lao, hawa vijana
wanaopita hapa wanasoma, tunaogopa sana wasije wakajiunga na wao hapa
kula ganja,” alisema mama mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe
gazetini.
Ilidaiwa kuwa msanii huyo pamoja na wenzake wamekuwa na kawaida ya
kukaa katika kijiwe hicho kila siku na kuvuta bangi huku baadhi yao
wakitumia madawa ya kulevya.
Baada ya kutiwa nguvuni kwa vijana hao, wakazi wa maeneo hayo
wamewamwagia sifa Mkuu wa Kituo cha Polisi Mabatini aliyefahamika kwa
jina moja la Mapunda kwa jinsi alivyofanikisha askari kuwahi eneo hilo
la tukio.
“Tulipopiga simu polisi, hatukutegemea kama ingekuwa haraka hivyo,
tunashangaa baada ya muda mfupi, wakaja eneo hili, kwa kweli huyu mkuu
ni mfano wa kuigwa, maana siku hizi likitokea tukio lolote lile ni
dakika chache gari limefika,” alisema mkazi mmoja wa eneo hilo.
Ferooz, mkali wa kibao cha Starehe baada ya kufikishwa kituoni hapo
alichukuliwa maelezo yake kabla ya kuwekwa rumande. Hadi gazeti hili
likienda mitamboni haikufahamika siku ya kufikishwa mahakamani kwa
wahalifu hao.
--GPL