MKURUGENZI wa zamani wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ameshinda kesi ya kukutwa na simu
gerezani iliyokuwa inamkabili hivi punde katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jijini Dar es Salaam.
Liyumba ameshinda kesi hiyo baada ya
upande wa Jamhuri na mchunguzi wa kesi hiyo kushindwa kuithibitishia
mahakama kuhusu tuhuma hiyo.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi,
Augustina Mmbando kuanzia saa 3:30 mpaka 4:20 asubuhi.

Amatus Liyumba na wapambe wake wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kushinda kesi.
