BETTY MKWASA NA MUMEWE CHARLES MKWASA WASHEREHEKEA MIAKA 25 YA NDOA YAO

 Wana Silver Jubilee, Betty Mkwasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma na mumewe Charles Boniface Mkwasa 'Master' Kocha msaidizi wa Yanga, wakionesha hati maalum ya ndoa kutoka kwa Papa Francis. Hati hiyo ya heshima hutolewa na Papa kwa wanandoa waliotimiza miaka 25 ya ndoa yao. Mkwasa na mkewe walitimiza miaka 25 ya ndoa yao Januari 14 mwaka huu na jana Januari 18 kuafanya misa maalum ya kubariki ndoa yao na kurejea viapo vyao vya ndoa.
Wakulima na wananchi kutoka Bahi ambako Mheshimiwa Betty Mkwasa anafanyia kazi walileta kuku wa kienyeji na mafuta ya alizeti lita zaidi ya 30, Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo, bata Mzinga na nafaka za mahindi na mchele kwa maharusi.  
   Baadhi ya wakuu wa Wilaya za mkoa wa Dodoma wakiwa na wake zao wakipiga picha na maharusi. Wa tatu kulia ni Mbunge wa Bahi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo