Matukio
ya kutisha yamezidi kuchukua sura mpya nchini Brazil baada ya mtu mmoja
asiyefahamika kukutwa akiwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha
baada ya mwili wake kukutwa akiwa amenyongwa bafuni.Mtu huyo inasemekana
amekaa kwa muda mrefu akiwa amefariki bila majirani zake pamoja na
ndugu zake kujua kuwa amekufa kwani mwili wake ulikutwa umeharibika
sana.
Haijaweza kufahamika mara moja kuwa aidha mtu huyo alinyongwa au yeye mwenyewe aliamua kujinyonga akiwa anaoga bafuni.

Wataalam
wa jeshi la polisi walieleza kuwa wanashuku kuwa huenda mtu huyo
alinyongwa kwa sababu si hali ya kawaida mtu kujinyonga akiwa anaoga
huku amevua nguo,ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa mtu huyo
alikuja kudhuriwa na watu wasiofahamika wakati alipokuwa akioga bafuni
kwake.
Nao majirani wa marehemu huyo walisema kuwa hawakuwahi kuona wala kuhisi uwepo wa jirani yao huyo mpaka baada ya muda mrefu kusikia harufu kali ikitoka nyumbani kwa mtu huyo,ndipo walipoamua kutoa taarifa kituo cha polisi kilichopo karibu yao ili hatua zaidi za kisheria zichukuliwe ndipo polisi walipowasili kwenye nyumba hiyo na kumkuta mtu huyo akiwa ameoza kabisa mwili mzima.