NDEGE ILIYOTUA KWA DHARURA UWANJA WA NDEGE ARUSHA YATOLEWA KWENYE TOPE


MAGARI mawili  kutoka kampuni ya Flying Cargo ya Arusha na Simba Trucking leo alasiri yalifanikiwa kuinasua ndege ya shirika la ndege la Ethiopia, Boeing 767 iliyokjuwa imenasa katika tope la uwanja wa ndege wa Arusha.

Magari hayo mawili  yenye winch T.897 APE na T. 958 AKS yalianza kazi hiyo saa 8.10 alasiri na kuiweka katika eneo la lami saa 9.02 alasiri.

Kabla ya kuvutwa, ndege hiyo ilikaguliwa na wakaguzi sita  wa ndege kutoka nchini Ethiopia na wawili wa Tanzania. Itakaguliwa tena na huenda ikaruka kesho. --- [via blogu ya Beda Msimbe, Lukwangule Ent.]


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo