MABANDA YA WAFANYABIASHARA NYUMA YA STENDI NJOMBE YAANZA KUBOMOLEWA



 Zoezi la Ubomoaji wa Mabanda Ukiendelea
 Na Gabriel Kilamlya Njombe

Hatimaye Serikali Mjini Njombe Imeanza Kutekeleza Zoezi la Ubomoaji wa Mabanda ya Wafanyabiashara wa Vyakula na Nguo Aina ya Mitumba Yaliyopo Nyuma ya Kituo cha Mabasi Mjini Njombe Katika Kuuweka Mji wa Njombe Katika Hali ya Usafi na Usalama Zaidi.

Hatua Hiyo Imekuja Kufuatia Kituo Hiki Kufuatilia Kwa Ukaribu Utekelezaji wa Zoezi Hilo Lililo Takiwa Kutekelezwa Tangu Mwezi Novemba Mwaka Huu Jambo Ambalo Lilishindwa Kufanyika.

Akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Edwin Mwanzinga Amesema Kuanza Kutekelezwa Kwa Zoezi Hilo Iwe ni Muendelezo wa Kuhakikisha Eneo Hilo Linakuwa Safi na Hivyo

Ameutaka Uongozi wa Mtaa wa Gwivaha Mjini Njombe Pamoja na Mambo Mengine Bwana Mwanzinga Amesema Kuwa Eneo Hilo Kwa Akali Kubwa Lilikuwa Likitumika Kwa Mambo Ya Uhalifu Ikiwemo Kutumika Katika Utumiaji wa Madawa ya Kulevya,Ulevi na Kutumia Kama Vyoo.

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Gwivaha  Mjini Njombe Bwana Nathanael Maxona Amesema Kuwa Ifikapo Disemba 19 Mwaka Huu Siku ya Alhamisi Zoezi Hilo Litakuwa Limekamilika Kwa Kuyaondoa na Kuyapanga Mabanda Hayo Kulinga na Biashara Wanazo Zifanya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo