Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
WAKAZI wa mjini hapa wamekilaani kitendo cha askari wa kituo kikuu cha polisi baada ya kumpa kipondo na kumkwida hadi kumvua nguo hadharani dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Bello.
WAKAZI wa mjini hapa wamekilaani kitendo cha askari wa kituo kikuu cha polisi baada ya kumpa kipondo na kumkwida hadi kumvua nguo hadharani dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Bello.
Polisi akimpa kichapo dereva daladala.
Tukio hilo lililojaza umati wa watu lililoshuhudiwa na paparazi wetu
lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya stendi ya daladala mjini
hapa.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema Bello aliyekuwa akiendesha gari aina
ya Toyota Hiace inayofanya safari zake kati ya Mjini na Mazimbu,
alikamatwa kwa kudaiwa kuegesha gari vibaya.
“Stendi ni ndogo Bello aliegesha gari lake akisubiri foleni yake ili
apakie, cha ajabu askari akafika na kumpa kibano kabla ya kumsweka
ndani,” alisema Wamaga Juma na kuongeza:
“Wananchi wenye hasira walitaka kumzingua askari yule, akapiga simu
na kuwaita wenzake wa kikosi cha usalama barabarani, walipofika
walimbeba Bello na kumpeleka kituoni huku akiwa na kipensi tu.”
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliwapongeza askari hao kwa madai
kuwa, madereva wengi wamekuwa wakivunja sheria za barabarani hivyo
kibano alichopewa Bello kitakuwa fundisho kwa wengine.
-GPL