WATU 17 WAJERUHIWA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUPINDUKA WILAYANI KAHAMA

Watu 17 wamejeruhiwa baada ya gari la abiria walilokuwa wakisafiria kutoka ulowa kwenda mjini kahama kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Nyandekwa wilaya ya kahama mkoani Shinyanga.
Miongoni mwa majeruhi waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama baada ya ajali
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi ikilihusisha gari namba T 208 AGE lilokuwa likiendeshwa na dereva aliyetajwa kwa jina la Rashid Ramadhan mkazi wa Kahama mjini, ambaye hata hivyo alitoroka baada ya tukio hilo.

Kwa mujibu wa daktari mfawidhi wa hospital ya wialaya ya Kahama, Deogratius Nyaga, jumla ya majeruhi 5 wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa huku 12 wakiwa wanaendelea na matibabu hospitalini hapo.
Daktari mfawidhi wa hospital ya wilaya ya Kahama, Deogratius Nyaga akiongea na waandishi wa habari
Daktari Nyaga amewataja waliolazwa kuwa ni Elizabert Mgesa (49), Katarina Makoye (32), Eliza Timotheo (30), Ngeke Chanila (23), Zawadi Andrea (18), Amos Hussein (32) na Adam John (20) ambaye alikuwa kondakta wa gari hilo. 

Wengine ni Zakaria Leonce (25), Mabala Paulo (28), Hamis Makala (26), John Marcel (26) na Michael Rashid (47) na motto benad Paulo mwenye umri wa miezi mitano na kwamba wote hali zao zinaendelea vizuri.

Jeshi la Polisi wilayani kahama limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uchunguzi wakubaini chanzo chake unafanywa, huku juhudi za kumtafuta dereva wa gari hilo zikiendelea.
Majeruhi akiwa na ndugu yake ambaye amekwenda kumtembelea
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa redio kahama fm akichukua maelezo kwa mama aliyejeruhiwa
Askari polisi akiwa akichukua maelezo kwa majeruhi kwenye wodi ya wanaume
Mama aliyejeruhiwa
Askari wa usalama barabarani akichukua amelezo kwa majeruhi kwenye wodi ya wanawake
Ajabu sana: Majeruhi wawili wakiwa katika kitanda kimoja
Mama aliyejeruhiwa pia katika ajali hiyo
Mgonjwa akiwa amepumzika baada ya kupatiwa huduma
Miongoni mwa waliopata ajali akiwa kitandani wodini
Dada huyu akiwa ametulia kitandani kumuomba mungu ampe ahueni
Majeruhi wawili katika kitanda kimoja kama inanvyoonekana
 Swali ni je ni hatua gani zinachukuliwa kuwakinga majeruhi kama hawa kutoambukizana magojwa hatari kama UKIMWI ilihali wanalala katika kitanda kiomoja na wote wana majeraha? 
 
Chanzo na mdau Faraji Mfinanga wa Dunia Kiganjani Blog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo