Watoto watatu wenye umri kati ya miezi mitano na miaka 13 wakazi wa
kitongoji cha Kibong'wa wilayani Kisarawe wamekufa papohapo baada ya
kufunikwa na kifusi cha udongo.
Watoto hao walifunikwa na kifusi hicho baada ya
wazazi wao kuwaweka katika eneo lililochimbwa kifusi awali ili wajikinge
na jua huku wao wakiendelea na kazi hiyo na ndipo ghafla kilipodondoka
kifusi kwenye eneo walilokuwepo watoto hao.
Mganga wa zamu kwenye hospitali ya wilaya Kisarawe Dkt, Hamza Mzige amethibitisha kupokea maiti za watoto hao Asnat Semeni(miezi mitano),Twaha Ally (2)na Mwazani Salehe(13),ambapo amesema
vifo vyao vimetokana na Kukosa hewa baada ya kufunikwa na kifusi hicho.
Majeruhi amina amiri ambaye hadi sasa hajafahamu
kupoteza maisha mtoto wake twaha allyaliyelazwa wodi namba nne
hsopitalini hapo amesema alikuwa amewaweka watoto hao ilikujikinga na
jua ghafla aliposikia kishindo na kuomba msaada.
Mkuu wa wilaya Kisarawe Fatuma Kimario aliyefika
hospitalini hapo amesema machimbo hayo ya Muilembe serikali ilipiga
marufuku na kubandika mabango ya kukataza na watu wamekuwa wakijiiba
kwenda kuchimba kokoto.
Itv iliyokuwepo katika eneo hilo ilishudhudia
kuwepo ukimya mkubwa baada ya wachimbaji wengi kukimbia eneo hilo
wakiogopa kukamatwa na kuacha vifaa vyao vya kazi.
Chanzo:ITV
