WASAKWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI MKOANI MBEYA

Jeshi la polisi Mkoani hapa linawatafuta Mama na Mtoto wake kwa tuhuma za mauaji ya Silevesta Alfonsi (55) mkazi wa Ichesya Wilayani Chunya mkoani hapa ambaye ni mume wa mtuhumiwa.

Akizungumzia kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi Mkoa huu kamishina Msaidizi wa polisi Diwani Athumani (Pichani) alisema Kurusina Korineli (42) na Mwanaye Kondo Silivesta (19) walimshambulia marehemu kwa kumpiga Rungu kichwani na na Utosini pamoja na ngumi na kumsababishia kifo chake papo hapo na watuhumiwa walikimbia walipobaini wameua.

Kamanda Athumani alisema inasadikika kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi kufuatia marehemu kuongea na mwanamke mwingine wakati wakiwa kilabuni na mbinu waliotumia ni kumshambulia kwa kumpiga baada ya kufika nje ya nyumba wakitoka kwenye kilabu cha pombe za kienyeji.

Ripota wa blog hii ya eddy blog Saimeni Mgalula amesema kuwa Tukio hilo lilitokea Novemba 12 mwaka huu saa 2:oo asubuhi kijijini hapo na Jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watuhumiwa waliotenda tukio hilo ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya dola kujibu mashtaka yanayo wakabili.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo