HALMASHAURI ZOTE NCHINI ZATAKIWA KUWA WAZI KWA WANANCHI WAKE

Na Saimeni Mgalula,Mbeya

Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI,imezitaka Halmashauri za Wilaya hapa Nchini kutenda kazi kwa uwazi kwa kuwajulisha Wananchi mambo zinazofanya ili waweze kutambua mchango wa Serikali kulinganisha nguvu zao.

Kauli hii ilitolewa jana na Waziri wa wizara hiyo Hawa Ghasia alivyokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya katika ziara ya siku moja na kuongeza kwamba Fedha zinapoletwa kwenye Halmashauri si siri ya Mkurugenzi na Watendaji wake bali Wananchi wanapaswa kujua.

Alisema malengo ya ziara yake ni kuja kuona jinsi Halmasharli zinavyofanya kazi iwapo zinafuata kanuni za uendeshaji kwa kufuata vikao stahili vya Madiwani na iwapo taarifa zinatolewa kwa madiwani ni sahihi 

Waziri Ghasia alitoa mfano kwamba kitendo cha kutompata mwenyekiti wa kijiji cha Mpemba pamoja na Wananchi wake katika mradi wa Nyumba ya Mwalimu si kizuri kwani alitegemea taarifa inayosomwa ya ujenzi huo pia Wananchi wasikie.

Alisema faida ya Wananchi kushiriki katika shughuli kama hizo ni kuweza kuelewa iwapo yale yanayozungumzwa kama yana ukweli gani.

Pia Serikali imetoa tamko linaloondoa Mkanganyiko uliokuwepo kuhusu uanzishwaji wa Halmashauli ya Mji mdogo wa Tunduma kwamba bado ni mamlaka ya mji mdogo wa Tunduma na si Halmashauri kamili kutokana na kukosa sifa.

Waziri Ghasia alitoa maelezo haya siku hiyo hiyo alipokuwa akiongea na Watumishi wa Halmashauri hiyo Mkoani hapa katika Ukumbi wa Halmashauri iliyopo kijij cha Ukwire

Alisema uanzishaji wa Halmashauri ya mji wa Tunduma na nyingine nne hapa Nchini haukuweza kufanikishwa kutokana na Halmashauri hizo kukosa sifa ya kutokuwa na Madiwani ambao ndio wanaounda baraza la madiwani.

"Hivi sasa katika mji wa Tunduma ni mamlaka ya mji mdogo ambayo inajukumu la kuendelea kupanga mji ikiwa ni pamoja kuandaa maeneo ya Utawala kwa kuunda hata kama  ni mpya ambazo baada ya uchaguzi watapatikana Madiwani hivyo itakuwa imekithi vigezo" alisema Ghasia.

Alizitaja baadhi ya Halmashauri hapa Nchini ambazo pia zipo katika kundi hilo ni pamoja na Handeni, Nzega na Kasuli ingawa alisema Halmashauri ya Nzega pekee ndiyo imetimiza vigezo baada ya Viongozi wao kufanya mbinu za kuunganisha kata za jirani.

Hata hivyo awali Afisa Mtendaji wa Mji wa Tunduma Aidani Mwashinga aliiomba Serikali kuajiri watendaji wa kata na mitaa ili kurahisisha utendaji kazi kutokana na kwamba mji huo una idadi kubwa ya watu ambao kwa mfumo uliopo inaonekana haina serikali kwa kuwatumia wenyeviti wa Vitongoji.

Alitaja idadi ya wakazi katika mji huo kuwa inakaribia watu 120,000 ambao wamekuwa wakitegemea kupata huduma moja kwa moja kutoka Ofisi ya Mtendaji wa Mji.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa huo Abbas Kandoro akijibu ombi hilo aliitaka mamlaka ya mji huo kuendelea kusubiri wakati serikali inaendelea na mchakato wa kuanzisha maeneo tawala isipo kuwa suala la Watendaji litaangaliwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo